Mr
Denis Kapama
alizaliwa mnamo tarehe 28/12/1964. katika kijiji cha jelemanga. wilaya ya Mpanda Zamani mkoa wa
Tabora baadaye Rukwa na sasa ni Katavi akiwa ni mtoto wa saba katika familia ya
watoto kumi na mbili wa Mzee Vitalis Kapama na Bi Juliana mucodemu Kisaye. Mr Denis kapama alibatizwa katika kanisa la parokia ya milala mnamo mwaka
1965. Alipata mafundisho ya komuniyopamoja na kipaimara.
Mr Denis kapama alianza safari yake ya
kutafuta elimu mnamo mwaka 1977 mpaka 1983.Alipo hitimu elimu yake ya msingi
katika shule Kasokola pia akajiunga na elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1984 mpaka katika shule ya
sekondary Kantalamba High School. Alijiunga na kidato cha sita {A-level} mwaka
1988 mpaka 1990 katika shule ya sekondari
Sengerema High School mnamo mwaka 1990.Baada ya hapo Mr Kapama alijiunga na jeshi la kujenga
Taifa {JKT} kwa mujibu wa sheria
katika kambi ya jeshi ya Itende mkoani Mbeya na kumalizia mafunzo yake makao
makuu ya JKT mlalakuwa Kawe jijini Dar es salaam.Akajiunga na elimu
ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaama kuanzia mwaka 1993 na kuhitimisha
shahada ya uwalimu mnamo mwaka 1997.
Mda wote huwo Mr Kapama alikua
akijisomesha uku akifundsha shule ya aga khan. Mwaka 2010 mpaka 2012 Mr Kapama
alipata alipata shahada ya Uzamili ya uwalimu {Masters of Education} katika
chuo kikuu cha Dar es saalam,Mwaka 2013 mpaka 2015 alitunukiwa shahada ya
kwanza ya Sheria katika chuo kikuu cha Bagamoyo University,vilevile Mr Kapama kwa juhudi zake za kusoma alitunukiwa
tena shahada uzamili ya sheria {Masters of Laws} katika chuo cha Bagamoyo
University mnamo mwaka 2013 mpaka 2015.
Mr
Kapama
aliajiliwa katika shule ya sekondari ya Aga Khan Mzizima,Mnamo mwaka 1997 mpaka
2000. Mwaka 2000 aliajiliwa katika shule ya Dar es salaam Independent International School iliyopo Mikocheni katika
jiji la Dar es salaam ambapo alidumu kwa miaka michache. Mwaka 2002 Mr Kapama
aliamua kujiajili mwenyewe kwa kuanzisha kituo cha elimu ya watu wazima na
ushauri nasaha cha TANGANYIKA EDU-CONSULT
CENTRE {TECC} ambacho kilianzishwa maeneo ya mwenge na baadae kuhamia sinza
mori na sasa kituo hiko kipo survey.
Alikuwa ndio mkuu wa kituo hiko pia mwalimu wa baadhi ya masomo ambayo nayo ni
English Language, Literature, General Studies
pia na Geography. Mr denis pia alikua vile vile akiwa ni mlezi mlezi wa
PAN AFRICANISM,Tanganyika chapter
na mchambuzi wa vipindi mbalimbali vya
redioni pia kwenye luninga kama vile E-FM
na CLOUDS FM kama mtaalam wa sheria na maswala ya kijamii.
Mr
Denis Kapama
aliishi vizuli na jamii yote iliyo mzunguka na alikuwa amejaliwa moyo wa huruma
na kujitolea katika kusaidia watu wenye shida/uhitaji vilevile alijitoa kwenye
kutoa elimu na kuzalisha wasomi wengi hata wale waliokua wamekata tamaa ya
kupata elimu aliwezakuwatia moyo na
kuwasaidia kupata elimu mchango huo mkubwa umekuwa chachu kubwa ya maendeleo
kwa jamii inayo mzunguka na Taifa kiujumla. Mr Denis alikuwa mstari wa mbele
katika kupigania haki na uongozi bora kwa kutoa elimu ya kijamii kwa watu wote waliomuhitaji
na waliomzunguka .
Mr
Denis Kapama
alifunga ndoa na Rose Chuku mnapo mwaka 12/7/1997 katika kanisa la St.Joseph,
liliopo posta jijini Dar es saalam na
kubalikiwa kupata watoto wanne wote wakiume nao ni Vitalis,Kisaye,Joseph na
Afrika .
Mr
Kapama
alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukali kuanzia mwaka 2009 katika muda wote
huo wa ugonjwa Mr Kapama akipata tiba katika hospitalize MUHIMBILI ,CCBRT na TUMBI kwa kipindi chote hicho aliendelea
kuimarika kiafya kwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa , Tiba na ushauri
kutoka kwa madaktari mnamo tarehe
12/1/2020 .
Mr Kapama alikuwa na furaha. Ilipofika
jioni aliwaambia watoto wake wote wanne pamoja na mtoto wa shemeji yake wakae
kikao ili kujadili mapungufu yao. Nao watoto kwa nidhamu ya juu walitii walikaa
kikao na kukosoana mabaya na kuchekeshana. Mr
kapama alivoona hivo aliwanunulia soda watoto wote. Baada ya mda kidogo
alianza kulalamika kwamba kifua kinamuuma. Usika wa saa nne alikimbizwa
hospitali na kuchomwa sindano baada ya hapo alirud nyumban na kupumzika kwa nje
akiwa na mke wake,shemeji yake watoto wake wawili Kisaye na Jose pia na Fauster
mtoto wa shemeji yake . Alikuwa akicheka nao na ghafla mida ya saa saba usiku
Mr Kapama alifaliki mbele ya Familia yake.walijitahidi kumuwahisha hospitali
lakini MUNGU alipenda Mr Denis Kapama apumzike kwa amani tangu usiku huo wa tarehe 13/1/2020.
3 Comments