TANGANYIKA OPEN SCHOOL
Karibu TECC,
Kituo
cha Habari Elimu na Ushauri cha Tanganyika (Tanganyika Edu-Consult Centre) ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyo na
usajiri kamili serikalini. Moja katika malengo yake ni kupambana na adui ujinga
kwa watu ambao kwasababu mbalimbali hawakupata au kukamilisha hatua mbalimbali
za elimu ya sekondari. Elimu hii ya kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita
kupitia mfumo usio rasmi hutolewa na kituo chini ya usimamizi na ushrikiano na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Wanafunzi wetu husoma kwa muda mfupi na
mrefu kutegemea kiwango cha uelewa wa mlengwa. Kwa wenye uelewa wa haraka,
huhitimu elimu ya kidato cha nne kwa miaka miwili na kwa wale wa kidato cha
sita kwa mwaka mmoja tu kwa kufanya mitihani ya taifa ya Baraza la Mitihani Tanzania (BAMITA/NECTA) kama watahiniwa wa kujitegemea (Private
Candidates)
TECC si kituo cha mitihani kwa hivi sasa.
Hata hivyo, taasisi hi iko kwenye mchakato wa kuomba kituo cha mitihani kwa
ngazi zote yaani QT, Kidato cha nne na kidato ch sita. Tunaendelea kuwasiliana
na BAMITA/NECTA kupitia Taasisi ya Elimu ya Elimu ya Watu Wazima ili
kukamilisha taratibu za kupata kituo cha Mitihani.
Mbali na shughuri za taaluma Kituo cha Habari Elimu na Ushauri cha
Tanganyika kinatoa huduma za ushauri na malezi (Guidance and Counseling)
bure na kwa kuzingatia maadili ya ushauri yakiwemo kutunza siri.
Shughuri hizi za Ushauri na taaluma
zinaendeshwa hapa makao makuu Makao Makuu, Barabara ya Kuelekea Chuo Kikuu Cha
Ardhi, Nyuma ya Hoteli ya Essaurp Village, Eneo la Savei, Mlalakuwa (Zamani –
Mlalakuwa Club), Kitalu Namba 249/, jijini Dar es Salaam.
Malipo yanafanywa kwa fedha taslimu kituoni
au kwa njia ya benki. Malipo kwa njia ya benki yafanywe kupitia
akaunti ya kituo yenye jina la Tanganyika
Edu- Consult Centre, Akaunti Namba 0152556699000
ya benki ya CRDB. Baada ya malipo
kupitia benki, mwanafunzi au mteja aje na stakabadhi (pay slip) ya benki
kituoni TECC.
Mwaka wa masomo unaanza tarehe 3 January na yapo madarasa ya Asubuhi (saa 2:00 – 8:00) na ya Jioni (saa 9:00–1:30). Madarasa ya Asubuhi hujaa mapema, hivyo kwa mwanafunzi anayetarajia kusoma darasa la asubuhi anashauriwa kujiunga mapema zai
FAIDA 10 ZA KUSOMA TECC
Wanafunzi
wanaosoma kituo hiki hunufaika na mambo makuu kumi kama ifuatavyo:
1. Wanafunzi wetu wanasoma kwenye kituo chenye
kutambuliwa na Wizara ya Elimu kupitia Usajiri na Usimamizi wa Taasisi ya Elimu
Ya Watu Wazima. Hii inafanya taasisi izingatie viwango vilivyowekwa na wizara
ikiwemo sifa za walimu. Walimu wetu hukaguliwa na Wizara ya Elimu kupitia
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
2. Wanfunzi wetu wanansajiliwa na wizara
kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na hivyo hufanya mitihani ya Utamilifu
ili kujipima na wanafunzi wengine nchi nzima kabla ya kufanya mitihani ya
taifa.
3. Wanfunzi wetu wananapewa vyeti vya kuhitimu
au Leaving Certificates) zinazotolewa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na
hivyo chini ya Wizara ya Elimu. Vyeti hivi vinatabulika na mamlaka zote nchini
na nje ya nchi.
4. Wahitimu wetu wa kidao cha nneambao hufaulu
hupewa fursa ya kujaza fomu za kozi mbalimbali, yaani Selection Form au Sel-form na hivyo kuchaguliwa kwenda kidato
chatano kwenye shule za serikali, Vyuo vya Ufundi stadi yaani VETA, Vyuo vya
ualimu na Chuo cha Polisi Moshi sawa na wale wanaosoma shule za serikali.
5. Wanfunzi wetu wanapata huduma ya ushauri na
malezi, yaani Guidance and Counselling bure. Elimu hi inahusu mabadiriko ya
mwili, Elimu ya ukimwi, Elimu ya uzazi na uchaguzi wa kozi za elimu ya juu,
n.k.
6. Wanfunzi wetu wanapata fursa kujifunza kwa
vitendo kupitia safari za kimasomo au Study Tours, semina za wataalamu
mbalimbali kutoka nyanja kadhaa kama vile siasa, michezo, mazingira, historia,
sanaa, uongozi wa serikali ya wanafunzi, nk. Vile vile hii ni njia ya kutambua
vipaji na mwelekeo wa kitaaluma na kimaisha.
7.
Wanfunzi
wetu hasa wale wa QT hupewa kozi maalumu ya Kiingereza ya mizi mitatu ili kuwasaidia wasio na msingi wa lugha hii
ambayo ni ya kufundishia na kujifunzia.
8.
Wanafunzi
wetu wanafundishwa na walimu wenye weledi, uzoefu na ari kubwa ya kujitolea.
Kwa eengi wao kufundisha si ujuzi na kazi tu bali pia ni mapezi au hobby.
9.
TECC ni
kimbilio la watu wenye uwezo mdogo kimapato. Gharama za ada na michango mingine
ni ndogo na inalipwa kwa awamu (instalments). Vilevile TECC ina mpago maalumu
wa kusaidia wsiojiweza kwa kuwaondolea sehemu ya ada au ada yote.
10. Wanajumuiya wote wa TECC aani wanafunzi,
walimu na wafanyakazi wasio walimu wanaishi kama familiya moja. Tukio la furaha
au majanga linalomsibu mmoja wetu huwaungnisha wanajumuiya wote katika
kulishughurikia kwa hali na mali. Tunashirikiana kwenye magonjwa, misiba,
harusi, dharula za ajali, moto n.k.
11. Wanafunzi wetu wanasoma kwenye kituo chenye
huduma za maktaba ndogo ambayo huwapa fursa ya kuazima vitabu vya kiada na vile
vya ziada.
12. TECC ni kituo kinachoendeshwa kwa misingi ya
democrasia kwa ktambua haja na umuhimu wa wanafunzi kuwa na serikali ya
wanafunzi ambayo huwa kiungo kati ya uongozi mkuu na wanafunzi.
* Ada na michango hiyo hapo juu haihusu usajili wa Mitihani ya Taifa.
SIKU
|
MUDA
|
JUMATATU-IJUMAA
|
ASUBUHI: SAA 2:00 – 8:00
JIONI:
SAA 9:00 – 9:30
|
MASOMO YANAYOFUNDISHWA· HAKUNA MASOMO SIKU ZA SIKUKUU NA WEEK END
MASOMO
|
||
No
|
O- LEVEL
|
A- LEVEL
|
1.
|
CIVICS
|
|
2.
|
HISTORY
|
|
3.
|
GEOGRAPHY
|
ARTS (ALL)
|
4.
|
KISWAHILI
|
|
5.
|
ENGLISH LANGUAGE
|
SCIENCE (ALL)
|
6.
|
LITERATURE IN ENGLISH
|
|
7.
|
BASIC MATHS
|
BUSINESS (ALL)
|
8.
|
BIOLOGY
|
|
9
|
COMMERCE
|
|
10
|
BOOK KEEPING
|
IDARA ZA KIUTENDAJI
Kituo cha Habari Elimu na
Ushauri cha Tanganyika
(Tanganyika Edu-Consult
Centre) ni Taasisi
inayotekeleza shughuri zake kupitia idara sita kama
ifuatavyo:
1.
Idara ya Elimu: Idara hii inashughurikia na kusimamia elimu ya sekondari na Elimu ya juu.
2.
Idara ya Malezi na Ushauri: Idara hii inashughurikia na kusimamia
utoaji wa ushauri na malezi (au Guidance and Counselling)
3.
Idara ya Ustawi wa Jamii: Idara hii inashughurikia na kusimamia mambo
yote ya kijamii yakiwemo matukio yote ya furaha au maafa yanayomkuta
mwanajumuiya. Vile vile hushirikiana na mamlaka za kijamii na za kiserikali
katika kutoa huduma na elimu katika majanga au maafa.
4.
Idara ya Kupambana na Umaskini: Idara hii inashughurikia shughuri zote
zinazolenga kundoa umaskini hasa kupitia elimu na uhamasishaji, kufanya tafiti
na harambe za kuwasaidia wenye uhitaji.
5.
Idara ya Elimu ya Afya ya Uzazi: Idara hii inashughurikia na kusimamia
utoaji wa elimu na ushaurijuu ya mambo yote yanayohusu afya ya uzazi, magonjwa
ya kuambukiza na kupanga uzazi.
6. Idara
ya Elimu kwa Umma: Idara
hii inashughurikia na kuratibu idara nyingine zote kwenye mambo yote
yanayohitaji uhamasishaji wa umma.
MAFANIKIO KITAALUMA
Taasisi hii
ilianzishwa kwa lengo moja kuu ambal ni kupambana na maadui wakuu watatu yaani
ujinga, maradhi na umaskini. TECC inaamini kwamba mwanzo mzuri wa vita hii ni
kuondoa kwanza ujinga na maadui wengine wawili wanaweza kutokomea kwa urahisi
zaidi.
Tangia
kuanzishwa kwake Aprili Mosi, 2002, TECC imefanikiwa kuwavusha maelfu ya
watanzania kutoka ngazi ya elimu ya msingi na kuingia na kuhitimu elimu ya
sekondari na vyuo vikuu. Na wengine kutoka elimu ya sekondari kwenda na
kuhitimu ngazi ya diploma na digrii. Kila chuo kikuu cha Tanzania kumekuwepo
wanafunzi ambao ni wahitimu wa kidato cha sita kutoka TECC.
Vile vile
TECC kupitia idara ya Malezi na Ushauri imefanikiwa kuwarekebisha tabia vijana
wengi na kuleta matumaini mapya kwenye family, jamii na taifa.
Watumishi
mbalimbali wa idara za serikali wakiwemo walimu, wauguzi , askari polisi katika mkoa wa Dar es Salaam wamesomea
TECC . Wengine ni wafanyabiashara/wajasiliamali, mama wa nyumbali watumishi wa
ndani, n.k.wamesomea TECC na kubadilisha historia zao za maisha.
Karibu katika ulimwengu wa
taaluma ili kutimiza ndoto yako. Tumekusudia na kujipanga vyema kubadili
historia na wasifu wako.
0 Comments