Karibu TECC,
Kituo
cha Habari Elimu na Ushauri cha Tanganyika (Tanganyika Edu-Consult Centre) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyo na
usajiri kamili serikalini. Moja katika malengo yake ni kupambana na adui ujinga
kwa watu ambao kwasababu mbalimbali hawakupata au kukamilisha hatua mbalimbali
za elimu ya sekondari. Elimu hii ya kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita
kupitia mfumo usio rasmi hutolewa na kituo chini ya usimamizi na ushrikiano na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Wanafunzi wetu husoma kwa muda mfupi na
mrefu kutegemea kiwango cha uelewa wa mlengwa. Kwa wenye uelewa wa haraka,
huhitimu elimu ya kidato cha nne kwa miaka miwili na kwa wale wa kidato cha
sita kwa mwaka mmoja tu kwa kufanya mitihani ya taifa ya Baraza la Mitihani Tanzania (BAMITA/NECTA) kama watahiniwa wa kujitegemea (Private
Candidates)
TECC si kituo cha mitihani kwa hivi sasa.
Hata hivyo, taasisi hi iko kwenye mchakato wa kuomba kituo cha mitihani kwa
ngazi zote yaani QT, Kidato cha nne na kidato ch sita. Tunaendelea kuwasiliana
na BAMITA/NECTA kupitia Taasisi ya Elimu ya Elimu ya Watu Wazima ili
kukamilisha taratibu za kupata kituo cha Mitihani kuanzia Januari 2015 kwa
wanafunzi wa kidato cha pili (QT) na cha nne, na kuanzia tarehe Mei 2016 kwa
wale wa kidato cha sita.
Mbali na shughuri za taaluma Kituo cha Habari Elimu na Ushauri cha
Tanganyika kinatoa huduma za ushauri na malezi (Guidance and Counseling)
bure na kwa kuzingatia maadili ya ushauri yakiwemo kutunza siri.
0 Comments